Wizara ilitoa kauli hiyo Ijumaa kufuatia tamko la pamoja la kundi la G7, linalojumuisha Marekani, Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, Italia, Kanada na Japan, pamoja na mkuu wa sera za mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya, Kaja Kallas, ambao waliituhumu Jamhuri ya Kiislamu kwa kuchukua kile kilichodaiwa kuwa eti ni hatua za ukatili dhidi ya waandamanaji wa masuala ya kiuchumi na hivyo kukiuka haki za binadamu.
Tamko la washirika hao lilipingana moja kwa moja na ushahidi mwingi uliopo nchini unaoonyesha ushiriki wa moja kwa moja wa Marekani na Israel katika kuyapotosha maandamano na kuyaelekeza kwenye vurugu, kama hatua ya awali kuelekea uwezekano wa mashambulizi mapya ya kijeshi dhidi ya nchi hiyo kama ilivyotishwa na Rais wa Marekani Donald Trump.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imepinga msimamo wa G7 na kusema kuwa kundi hilo limepuuza thamani ya ushahidi uliopo unaoonyesha kwamba maandamano ya amani katika Jamhuri ya Kiislamu yalisukumwa kwa makusudi kuelekea vurugu kupitia shughuli za kigaidi zinazoungwa mkono na madola ya kigeni.
Kulingana na wizara hiyo, mikusanyiko ya amani iliyofanyika kati ya Januari 8 na 10 ilivurugwa kwa uingizwaji uliopangwa wa vikundi vya kigaidi vilivyokuwa vimepatiwa vifaa na utawala wa Kizayuni wa Israel.
The Group of 7
Taarifa hiyo ilibainisha jinsi waliopenya kwenye maandamano walivyopanga mashambulizi dhidi ya waandamanaji na maafisa wa usalama, na kusababisha vifo vya waandamanaji wengi pamoja na maafisa wa usalama.
Taarifa hiyo ilinukuu matamshi ya wazi ya maafisa wa sasa na wa zamani wa Marekani na Israel yaliyolenga kuchochea vurugu na umwagaji damu kote nchini.
Habari inayohusiana:
Rais Pezeshkian Marekani na Israel zimehusika moja kwa moja katika machafuko Iran
Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imeongeza kuwa vyombo vya usalama vimekusanya “ushahidi thabiti na nyaraka” zinazoonyesha jukumu la moja kwa moja la utawala wa Kizayuni wa Israel katika kupanga na kuziandaa silaha kwa makundi ya kigaidi, kwa msaada wa Marekani.
Hapo awali, vyombo vya usalama vya Iran vilitangaza kuvunja mtandao wa kigaidi unaohusishwa na shirika la ujasusi la Mossad la Israel na kukamata shehena kubwa ya silaha zilizokuwa zimekusudiwa kutumika Tehran.
Your Comment